Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua
eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya
Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na
umeme.
Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu
Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji
inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea
na kikundi cha vijana Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili
ya kujiajiri kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe
wake wakikagua jengo la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa
maelekezo ya matumizi bora ya dari la jengo la biashara la Mukendo lililojengwa
na NHC katika Manispaa ya Musoma ili kuongeza mapato ya Shirika.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe
wake walipotembelea Wilayani Tarime kujionea nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC mwaka 1968 na ambazo hadi hivi sasa zinasaidia familia
mbalimbali. Nyumba hizi ni za vyumba viwili na zilipewa Halmashauri hiyo mwaka 1991.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadili namna
ya kuongeza ubora wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika maeneo
mbalimbali nchini. Amesisitiza kupunguza gharama ya ujenzi ili nyumba
zinazojengwa ziwe nafuu.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
ukiangalia mnara wa kumbukumbu ya mahali ambapo ilikuwepo nyumba aliyozaliwa
Baba wa Taifa.
Mojawapo ya nyumba aliyoishi Mwalimu Nyerere ambayo ilijengwa
1974 na aliyekuwa Rais wa Msumbiji Hayati Samora Moses Machel.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu aliwa
amekaa sehemu maarufu aliyokuwa akikaa Mwalimu Nyerere wakati wa kucheza bao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Isibania nchini Kenya kujionea namna nchi hiyo ilivyopanga eneo lao la mpakani.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Sirari kuona eneo la kujenga nyumba ili kuboresha taswira ya mpaka wa nchi yetu. Ujumbuliongozwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Tarime.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake pamoja naongozi wa Wilaya ya Butiama wakikagua eneo lililotengwa na Wilaya hiyo ili NHC ijenge nyumba za gharama nafuu. Bw. Mchechu amesisitiza kuwa NHC itajenga nyumba katika Wilaya hiyo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere wa kulianzisha Shirika la Nyumba la kwanza nchini Tanzania mwaka mmoja tu baada ya uhuru.
No comments:
Post a Comment