Saturday, January 24, 2015

KINANA APOKELEWA KWA MCHAKAMCHAKA WA NGUVU JIMBO LA DONGE

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kushoto  akipokelewa kwa mchakamchaka na Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu  Sadifa Juma Khamis wa tatu kutoka kushoto pamoja na vijana wa jimbo hilo ambao walikimbia naye umbali wa kilomita moja wakiwa katika mapokezi hayo yaliyotia fora mara baada ya kuanza ziara yake katika jimbo hilo leo akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DONGE-KASKAZINI UNGUJA B)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwa sambamba na Nape Nnauye katika mchakamchaka wakati wa mapokezi hayo katika jimbo la Donge Kaskazini Unguja.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  katikati, Mbunge wa jimbo la Dole Sadifa Juma Khamis wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Bakari Ame Hussein mwalimu mkuu wa skuli ya msingi ya Mahonda jimbo la Donge.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Awali Mahonda jimbo la Donge.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo wakati Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Dole mara baada ya kupokea mifuko 50 ya saruji kutoka kwa mbunge wao Sadifa Juma Khamis na Mabati 200 kutoka kwa Katibu Mkuu Abulrahman Kinana9Salum Gharib Salum Mwenyekiti wa kamati ya Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Misufini jimbo la Doleakishukuru mara baada ya kupokea misaada hiyo ya vifaa vya ujenzi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na  mbunge Sadifa Juma Khamis.10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na  mbunge Sadifa Juma Khamis wakishiriki ujenzi wa skuli ya Bumbwini Misufini.11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakikagua skuli ya skuli ya Mahonda.14Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo mara baada ya  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujezni wa ofisi ya CCM tawi la Muembe Jogoo.15Baadhi ya wanafunzi wa madarasa ya Amali  huko Kinduni jimbo la Kitope wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati alipokagua na kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya katika masomo yao .16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi majiko ya genzi ya kupikia kwa wanafunzi vijana wa madarasa ya Amali huko Kinduni jimbo la Kitope17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya mapishi..18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya ushonaji wa nguo.19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kazi za ushonaji huku  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiangalia shughuli mbalimbali za vijana wa mafunzo ya Amali katika mambo ya ushonaji wa nguo.21Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Maskani ya CCM Kizota jombo la Kitope.22Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.23Balozi Ali Karume akitema cheche zake kuhusu Katiba Mpya iliyopendekezwa na kuwashawishi wananchi waipigia kura ya ndiyo.24Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.2526Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika Maskani ya CCM Kizota.27Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Idd akiwahutubia wananchi wa jimbo la Kitope Kaskazini Unguja.28Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo na kuwsiki waipigie kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwa kuwa ina mambo mengi yenye faida kwa wazanzibari.29Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya mkutano huo kumalizika, Kushoto anayefurahia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...