Tuesday, January 20, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Katika ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari  katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR)2
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati alipowasili katika kijiji cha Dunga jimbo la Uzini mkoa wa Unguja Kusini jana.3
Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano wa ndani  pamoja na wawakilishi wenzake wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga. 4
Ndugu Sauda Mpambalyoto Katibu wa CCM wilaya ya Kati mkoa wa Unguja Kusini akisoma taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga jana.5
Kutoka kulia ni Balozi Ali Karume na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakiwa katika mkutano huo.6
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Unguja kusini.7
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Vuai Ali Vuai kumwaga zenge la linta kwenye jengo la CCM Dunga.
8
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki huko Unguja Ukuu jimbo la Koani.9
Baadhi ya wana CCM wakifurahia wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika soko la Unguja Ukuuu jimbo la Koani.10
Mwakilishi wa jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Gavu akizunguza wakati alipokabidhi misaada mbalimbali katika jimbo lake la Chwaka.11
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi jenzi kwa vijana wa jimbo la Chwaka
.12
Injinia Heri Tumaini Mkurugenzi wa kampuni ya CHECOTEC (T) LTD inayojenga barabara katika jimbo la Chwaka akishukuru na kuzungumza maneno yenye hisia ya furaha yake kwa kukutana na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.13
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la viungo la Alis Spices &Fruits Farm wakati alipokagua shughuli zinazofanywa katika shamba hilo lililopo Kwabani jimbo la Koani Zanzibar.14
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miche ya mikarafuu.15
Mmiliki wa shamba hilo Bw. Ali akizingumza na kumshukuru  katibu mkuu wa CC kwa kutembelea shamba hilo.16
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na mmiliki wa shamba hili pamoja na wafanyakazi.17
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye tanki la maji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo kijiji cha Michui jimbo la Koani Zanzibar.19
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni jimbo la Uzini.20
Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao kuashiria kuiunga mkono na kuipitisha Katiba mpya iliyopendekezwa.21
Mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa jimbo la Uzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni.22

23
Baadhi ya wawakilishi wa timu mbalimbali wakiwa na jenzi zao zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib.24
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Tunduni wakati wa mkutano wa hadhara,25
Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  wa kwanza kutoka kushoto akiwa  na wawakilishi wenzake wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kijiji cha Tunduni.26Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...