Wednesday, January 21, 2015

WAANDISHI WA HABARI KUJIONEA NA KUJIFUNZA ATHARI ZA VITA SUDANI KUSINI

DSC_0135
……………………………………………………………………………………………………………
Na Gladness Mushi-Ngurudoto Arusha
 Waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kuipelekwa nchini Sudan Kusini ili kujifunza athari za vita ambazo zimetokea katika nchi ya Sudani kusini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,leo wakati akizungumza na waaandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini  baina ya vikundi vinavyogombana kutoka nchini Sudani.
Kinana amesema kuwa baada ya kuwekeana saini na makubaliano ya kuacha mapigano basi Nchi ya Tanzania itachukua jukumu la kupekeka waaandishi wa habari Sudani kwa malengo  ya kujifunza na kujionea athari za vita .
“Tunataka waandishi wetu wa habari kutoka Tanzania wapate  uelewa wa kutosha katika kuandika na kutangaza madhara ya
vita vya wenyewe kwa wenyewe, Kinana aliahidi kuwa ni muhimu na atahakikisha
anawapeleka waandishi wa habari  waitembelee Sudan Kusini,”alisema.
Kinana alifafanua kuwa yeye binafsi anaamini watakapokwenda kujionea kwa macho madhara ya vita
wataweza kutumia vema kalamu zao kuelimisha watanzania madhara ya
vita.
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kiliombwa kufanya na kusimamia mazungumzo juu ya vita hiyo na ndivyo watakavyofanya
pia kwa waandishi ili wapate somo.
Alisema mapigano hayo yamesababisha uchumi wa nchi hiyo kurudi nyuma,
ukizingatia kuwa wao ni wazalishaji wakubwa wa ng’ombea na watatu
katika nchi za Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo pia wana utajiri mkubwa wa mafuta.
alisema Sudan Kusini ilihangaika miaka zaidi ya 50 kutafuta uhuru wao, miaka
miwili baada ya kujitenga kutoka Sudan Kaskazini, baada ya asilimia
90% kupiga kura ya kujitenga wakaanza vita ya kugombea madaraka, sasa
kila familia imeathirika kutokana vita ndio wanasaka amani.
Mazungumzo ya kutafuta amani kwa nchi hiyo yalianza mapema Desemba 23
na 24 mwaka jana 2014 katika Hotel ya Ngurudoto, Wilayani Arumeru,
Mkoan Arusha, huku zikiwakutanisha pande zote tatu zinazopigana kwa
ajili ya kusaka madaraka.
Katika mazungumzo hayo mwenyekiti wa mazungumzo hayo ni Balozi Dk.
John Samwel Malecela, ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu awamu
ya pili ya uongozi wa Rais Ally Hassan Mwinyi.
Mapigano hayo ya ndani ya chama cha SPLM katika nchi ya Sudani Kusini
yanahusisha makundi matatu ambapo kila kundi linataka madaraka ya
kuongoza nchi hiyo.

No comments: