Katika picha kulia Mwenyekiti mpya wa mtaa wa Kaloleni jijini Arusha Abdul Nassor juzi alikabidhi matofali 100 kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi kaloleni mama Raymond Pudensian kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shule hiyo inayokabiliwa na changamoto ya uzio
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kaloleni mama Raymond Pudensian akisoma taarifa ya shule kwa uongozi wa mtaa wa kaloleni baada ya mwenyekiti Abdul Nassor kukabidhi matofali 100 kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shule
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Bano akizungumza ambapo alisisitiza watu kujitolea kama alivtofanya mwenyekiti wa mtaa huo
Wanafunzi wakiwa wanasukuma mashine kwaajili ya kutengeneza kisima cha maji
Mwanafunzi mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa anaosha vyombo shuleni hapo
Hapa baadhi ya wanafunzi wenye tatizo la utindio wa ubongo wakiwa darasani
Picha ya pamoja
Wanafunzi wakiwa katika darasa la vitendo
……………………. |
Shule ya msingi ya kaloleni na makumbusho iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio shuleni hapo hali inayochangia utoro kwa wanafunzi.
Kutokana na changamoto hiyo mwenyekiti mpya wa mtaa wa kaloleni Abdul Nassor juzi alikabidhi matofali 100 kwa mwalimu mkuu wa shule ya kaloleni kwa ajili ya ujenzi wa uzio utakaotumika pia kwa shule ya msingi ya makumbusho
Mwenyekiti Nassor alisema aliguswa kuchangia mchango huo kutokana na hali halisi ya shule hiyo kukosa uzio hali ambayo pia kiusalama kwa wanafunzi wanaosoma hapo kuwa mdogo
Aliwataka wadau mbalimbali na hata waliowahi kusoma katika shule hizo kujitokeza kuchangia katika ujenzi wa uzio wa shule
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kaloleni mama Raymond Pudensian akipokea msaada huo alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya uzio shuleni hapo hivyo aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia matofali kwaajili ya ujenzi huo.
Bi Pudensiana alitaja makadirio ya matofali 5000 yanahitajika kwaajili ya uzio wa shule hiyo na kwa kukamilika kwa uzio huo itasaidia mauzurio mazuri kwa wanafunzi pamoja na usalama wa kutosha
‘’Kutokana na shule yetu kupakana na mto kwakweli hali ya kiusalama ni mdogo kwa kuwa hata wanafunzi wanaweza kwenda kujificha huko ila uzio ukikamilika itakuwa imesaidia kwa kiwango kikubwa”alisema Pudensiana
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
No comments:
Post a Comment