Wednesday, January 21, 2015

WILAYA YA RUFIJI YAPOKEA VIFAA TIBA

unnamed (1)Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akimshukuru Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
unnamed (2)Baadhi ya akina mama wakimshukuru Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid kwa kuwapatia vifaa tiba kuwalinda na kuimarisha afya ya mama na motto.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
unnamed (53)Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akiongea na wananchi wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.
unnamed (55)Diwani wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid kuongea na wananchi wa kata hiyo hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humounnamed (56)Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (kushoto) akiteta jambo na diwani wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba (kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
unnamed (57)Wananchi wa kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani wakimkasikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.
unnamedWaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (aliyevaa shati la batiki) akishirikiana na wananchi wa kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kufungua kitanda kwa ajili ya akinamama kujifungulia hivi karibuni wakati anakabidhi vifaa tiba kwa ajili ya wilaya hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni
…………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 23.8 ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na kitanda kimoja kwa ajili ya akina mama kujifungulia chenye thamani ya sh. Milioni 1.5, vitanda 50 na magodoro manne.
Makabidhiano hayo ya vifaa hivyo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati ya Nyamwage iliyopo kata ya Mbwala wilayani Rufiji huku yakishudiwa na wananchi wa eneo hilo wakiwa mashuhuda wa makabidhiano hayo.
Akikabidhi vifaa hivyo, Dkt. Seif aliwaasa wananchi wanaotumia zahanati hiyo kuvitumia na kuvitunza vizuri vifaa hivyo ili kupunguza tatizo la akina mama wajawazito kupata adha wakati wa kujifungua na wagonjwa wengine wanakaopata huduma katika zahanati hiyo.
Dkt. Seif alisema kuwa vifaa hivyo vinatokana na moyo wa wanarufiji waishio jijini Dar es salaam na marafiki wa Rufiji ambao wameanzisha mfuko wa Maendeleo wa Wanarufiji unaolenga kuinua maisha ya wananchi wa wilaya hiyo katika kusimamia upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo afya, umeme, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu, kilimo, biashara na ardhi.
Kuhusu suala la umeme, Dkt. Seif alisema kuwa mpaka sasa wilaya ya Rufiji vipo vijiji 39 ambavyo tayari vimeunganishiwa huduma hiyo ambapo taendelea kusaidia kuboresha vitu vingi akitolea mfano Nyamwage ilivobadilika na kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.
Na kwa upande wa huduma ya maji kwa wananchi wa Rufiji, Dkt. Seif alisema kuwa kamati ya mfumko wa maendeleo Rufiji kwa kushirikiana na marafiki wa Rufiji watachima visima zaidi ya 25 katika vijiji mbalimbali ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji salama na kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi waweze kujiletea maendeleo yao kwa kushirikiana na Serikali.
Dkt. Seif alibainisha kuwa umoja wa wanarujiji hao walifanya harambee mwaka jana jijini Dar es salaam iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt. Mohamed Gharib Bilal ambapo zilipatika sh. Milioni 900 ambapo lengo la harambee hiyo lilikuwa kukusanya sh. Milioni 1.5.
“Wenzetu wamejitahidi wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho katika harambee hiyo leo hii wanarufiji tunapokea michango ya wenzetu wanaothamini afya zetu na maendeleo ya wilaya yetu” alisema Dkt. Seif.
Aidha, Dkt. Seif alisema kuwa mfuko huo umeanzishiwa akaunti yake ambapo michango yote huwekwa pamoja na kamati husika inapanga ni vipaumbele vipi vifanyiwe kazi kwanza na ni kwa eneo gani la wilaya na kwa wakati gani.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia alisema kuwa kampuni yake imesukumwa na moyo wa kuwasaidia wanarufiji kwani yeye amesomea wilayani humo hivyo kampuni yake inathamini na itaendelea kusaidia masuala ya kiafya ambayo ndio kiini cha ufanisi wa maaenedeleo wilayani humo.
Kampuni hiyo katika kufanikisha utoaji wa huduma bora za jamii imechangia na kutoa vitanda 50, mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na kuahidi kutoa madawati 10 pamoja na pesa sh. Milioni 10.
Harambee ya kusaidia Rufiji iliyofanyika jijini Dar es salaam ilifanikishwa na kusimamaiwa na wanarufiji kwa kushirikiana na kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical na Jumuiya wa Kiislamu ya ISTIQAAMA.

No comments: