Monday, January 19, 2015

NHC yaendesha kongamano la kuwajengea uwezo wa kusimamia biashara Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine.

Mhadhiri Mwandamizi wa Biashara  wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Profesa Michael Munkumba akitoa mada asubuhi hii, kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akifungua kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki. Akizungumza katika kongamano hilo Maagi amesisitiza kuwa kongamano hilo linakusudia kujenga uwezo wa kiuongozi wa kusimamia mabadiliko ya kiutendaji na hatimaye kuwa Shirika la mfano siyo Tanzania tu bali Afrika na Duniani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akifungua kongamano hilo.

Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.

Washiriki wa kongamano hilo wakisalimiana wakati wakiwasili katika kongamano  hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs.

 Washiriki wa kongamano wakiendelea kufuatilia mada iliyotolewa na nguli wa mada ya mabadiliko katika Shirika, Prof. Munkumba.



 Washiriki wakiendelea kufuatilia mada katika kongamano hilo


Mameneja wa Mikoa ni sehemu ya wajumbe wa kongamano hilo. kutoka kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John, Meneja wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha na Meneja wa Ilala Bw. Jackson Maagi.

 Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia kwa umakini mada ya Prof. Munkumba


Mhadhiri Mwandamizi wa Biashara  wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Profesa Michael Munkumba akitoa mada asubuhi hii, kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs Hotel Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...