Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea maua kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Lilian Aroko mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (Kulia) akimpokea Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) mara waziri huyo alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria, Salome Makange mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Makao Mkuu ya Wizara.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini
No comments:
Post a Comment