Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous jana
Maelezo kuhusu masalia ya injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge
Waziri Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo
Waziri Nyalandu akisalimiana na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, David Feloemann, alipowasili kwenye mbuga ya Selous jana
Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous |
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous jana.
Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyama ya Selous jana
Waziri Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress
Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani
Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous
Askari wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili
Askari wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment