Wednesday, January 21, 2015

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS UMMY MWALIMU ZIARANI MKOA ARUSHA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais MhUmmy Mwalimu amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika baadhi ya viwanda vya Arusha lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu viwanda kutotumia magogo kama nishati ya uzalishaji viwandaniunnamed (31)Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Bw. Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea kiwanda cha A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.
unnamed (32)Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Bw. Binesh Haria Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha. Naibu Waziri alikuwa na ziara ya ukaguzi wa masuala ya Mazingira kiwandani hapo.
unnamed (33)Shehena ya magogo iliyobaki katika Kiwanda cha Sunflag. Kiwanda hicho kwa sasa kimebadilisha matumizi ya nishati ya uzalishaji kutoka kwenye magogo na kutumia makaa ya mawe.
unnamed (34)Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (Katikati) akipata taarifa fupi kutoka kwa kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani hapo kuangalia masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Mapunda.
unnamed (35)Moja ya boiler inayotumia makaa ya mawe katika Kiwanda cha Sunflag. Awali Kiwanda hicho kilikuwa kinatumia nishati ya Magogo katika shughuli za uzalishaji kiwandani hapo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya magogo ili kuhifadhi mazingira.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...