Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kwenye semina ya siku mbili iliyohusu matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuinua uchumi kupitia viwanda na uhifadhi wa mazingira na Sekta ya Umma kuimarisha ubunifu kwenye Sayansi hai.…
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kwenye semina ya siku mbili iliyohusu matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuinua uchumi kupitia viwanda na uhifadhi wa mazingira na Sekta ya Umma kuimarisha ubunifu kwenye Sayansi hai.
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), akichangia mada katika semina hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Banana Investment ya Arusha, Adolf Olomi, akizungumza na waandishi wa habari. Kampuni hiyo imefanikiwa kutumia maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho na kuyatumia kwa matumizi mengine kupitia utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo
Semina ikiendelea.
UKUAJI wa Sekta ya Sayansi na Teknolojia umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na msaada katika kuharakisha na kuboresha na urahisishaji wa kuleta maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya siku mbili iliyowakutanisha wanasayansi kutoka Afrika Mashariki iliyohusu matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuinua uchumi kupitia viwanda na uhifadhi wa mazingira na Sekta ya Umma kuimarisha ubunifu kwenye Sayansi hai iliyofikia tamati jana jijini Dar es Salaam jana.
"Katika hatua tulioifikia sekta hiyo kupitia Costech imeamua kukuza uchumi kwa kuboresha mazingira kwa kutumia maji taka ya viwandani ili yaweze kufanya kazi zingine hususan katika kilimo cha umwagiliaji" alisema Dk.Mshinda.Alisema lengo la semina hiyo ni kutafuta mbinu za kukuza ajira kwa vijana kupitia sayansi na teknolojia kupitia Costech na wadau wanayansi wengine.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka kitengo cha Uhandisi Kemikali na Usindikaji wa Madini, Profesa Juma Katima alisema kupitian sayansi na teknolojia wameweza kufanikiwa kubadilisha matumizi ya maji taka yanayotoka viwandani na kuyatumia kwa matumizi mengine.
"Tumefanikiwa sana katika hatua hii na kiwanda cha mfano ni kile cha Kampuni ya Banana Envestment cha Arusha ambacho kilikuwa kikizarisha mapipa ya maji taka ambayo sasa yameelekezwa kufanya kazi za kilimo na matumizi mengine" alisema Profesa Katima.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Adolf Olowi alisema hivi sasa kiwanda chake kimekuwa cha mfano wa kutunza mazingira baada ya wataalamu hao kufanya utafiti ulioleta mafanikio hayo ya kutumia maji taka kutoka kiwandani kwao. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment