Monday, January 05, 2015

Membe: Siwaonei wivu maswahiba wa mafisadi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamillius Membe akizindua sherehe ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, jijini Dar es salaam jana Jumapili, Januari 4, 2015, akishuhudiwa na  Dk. Valentine Mokiwa, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
 Waziri Membe akizungumza katika sherehe hiyo
 Askofu Mokiwa akitoa mahubiri katika ibada ya uzinduzi wa sherehe ya miaka 50 ya Diyosisi ya Dar es Salaam. .
 
 Waziri Membe akisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu Valentino
 Masista nao wakifuatilia 
 Waziri Membe aliaanza kumkabidhi kitabu cha Harambee Askofu Mokiwa
 Waziri Membe akikaribishwa na Askofu Mokiwa kwaajili ya utoaji wa vitabu vya kuchangishia fedha kwa ajili ya miradi ya Dayosisi

 Mwimbishaji kwaya (hayupo pichani)akiwaimbisha nyimbo wanakwaya waliovalia majoho ya rangi ya blue na nyeupe.

 Mwimbishaji kwaya akiwaimbisha nyimbo wanakwaya waliovalia majoho ya rangi ya blue na nyeupe.
 Wachungaji wakimsikiliza Mheshimiwa Membe kwa makini wakati akiongea.Picha na Reginald Philip
---
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema hapendi ufisadi na anajua mafisadi hawampendi lakini, hawaonei wivu watu wanaopendwa na mafisadi.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa la Anglikana Tanzania, ambayo alikuwa mgeni rasmi, Membe alitumia nafasi hiyo kuwataka waumini wa kanisa hilo kupambana na ufisadi katika ngazi zote nchini.
“Ninatosheka kupendwa na wale wenye mapenzi mema na Taifa letu. Sipendi rushwa na ufisadi. Ninashukuru Mungu kuwa rushwa, ufisadi na mafisadi hawanipendi zaidi,” alisema Membe.
Membe ambaye ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi, alisema si jukumu la viongozi pekee au chama fulani pekee kupambana na ufisadi, bali ni wajibu wa kila mmoja kwa kuwa mafisadi wako katika ngazi zote.
“Ninaamini, mwaka huu, wengi wetu tukisema hivyo, tukasimama katika mstari huo na tukaenda hivyo, ufisadi hauwezi kutushinda. Kila mmoja asipuuze udogo wa sauti yake au uchache wetu dhidi ya wale waovu, maana hata mwale mdogo wa mshumaa hufukuza giza,” alisema Membe na kuongeza:
“Wako wanaotoboa mtumbwi wetu tunaosafiria pamoja na jitihada zetu za kupiga makasia.”
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, Membe ambaye pia anatajwa kuwania urais, alisema mwaka huu ni wa kipekee si tu kwa dayosisi hiyo inayoadhimisha miaka 50, bali pia kwa Watanzania wote: “Mwaka huu una mambo makubwa mawili yaliyo mbele yetu, yaani kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu.
“Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu kwani tunachagua rais mpya atakayeunda Serikali mpya ya awamu ya tano ambaye anatarajiwa kuendeleza mema ya awamu ya nne na awamu zilizopita na kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo.”
Nchi majaribuni
Membe alisema nchi inapita katika majaribu na mitihani mikubwa kutokana na tatizo la mmomonyoko wa maadili katika ngazi zote kuanzia familia, shule, ofisini na serikalini.
“Tunalo tatizo la ufisadi, ukatili dhidi ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi na tunalo pia tatizo la umaskini. Tunalo tatizo la kupoteza uvumilivu wa kidini na kisiasa.”
SOURCE: MWANANCHI

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...