Thursday, March 05, 2026

Mhe. Ndejembi Akutana na Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta (TAOMAC)

 













Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) kwa lengo la kuboresha na kukuza sekta ya mafuta nchini pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta hiyo.

Kikao hicho kimefanyika leo, Machi 5, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika Kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha usimamizi, ufanisi na maendeleo ya sekta ya mafuta nchini kwa manufaa ya uchumi na wananchi kwa ujumla.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamishna wa Mafuta kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Goodluck Shirima; Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon; Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule; pamoja na viongozi na wanachama wa TAOMAC.

No comments:

WAZIRI MKUU: FEDHA ZA MUUNGANO ZITUMIKE KUKARABATI MIUNDOMBINU YA BARABARA

  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha ...