Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kwa Msanja kata ya Kibindu katika jimbo la Chalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho, ambapo viongozi kadhaa wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma wamewataka wananchi hao wa kata ya Kibindukumchagua mgombea ubunge wa CCM Bw. Ridhiwani Kikwete kwa kuwa anaweza kuwatatulia matatizo yao mbalimbali yanayowakabili katika kata yao kwani Ridhiwani Kikwete ni msomi, mwanasheria na mtu aliyepewa dhamana na chama cha Mapinduzi chenye uongozi kuanzia shina mpaka ngazi ya kitaifa hivyo wanao uwezo wa kumpata mahali popote kwani anao udhamini wa kuaminika. hata hivyo tatizo kubwa la kata ya Kibindu ni miundo mbinu ya barabara na maji jambo ambalo wananchi hao wanaeleza kwamba ni muhimu mbunge wao anayekuja aanze nalo, Mbunge aliyepita Marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo aliugua muda mrefu jambo lililopelekea wananchi hao kukosa mwakilishi wao katika mambo mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kwamsanja Kibindu leo.Hii ndiyo hali halisi msafara wa viongozi hao ukielekea kijiji cha Kwakirumbi kwa ajili ya mkutano wa kampeni kijijini hapo.Moja ya magari tuliyotumia likipita katika madimbwi makubwa.Gari hili likiwa limekwama na likisukumwa ili kunasua katika dimbwi la matope. Kwaya ikitumbuiza katika kijiji cha kwa Kirumbi.Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kijiji cha Kwamsanja.Wananchi wakiserebuka na muziki kjijini Kwakirumbi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.Mtela Mwampamba kutoka UVCCM makao makuu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.Ukaguzi wa barabara ukifanyika kabla ya kupita.Juhudi zikifanyika kunasua gari lililokwama.Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita akipita na gari lake katika madimbwi.Wananchi wakserebeka na muziki kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mjembe.Baadhi ya morani wa kimasai wakifurahia jambo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mjembe kata ya Kibindu.Hapa mambo yamekaa sawa tunakunja vifaa na tunang’oa nanga.Safari kuelekea kwenye magari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment