Picha juu haihusiani kwa lolote na ajali iliyotokea.
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba treni ya mizigo imepata ajali eneo la GodeGode mkoani Dodoma. Mtu mmoja anasadikiwa kufa huku wengine watano wakiwa hawajulikani walipo. Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba Treni hiyo ilisombwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Juhudi za kukinasua kichwa cha treni bado zinaendelea. Kwa habari zaidi na picha tutakuletea hivi punde.
Chanzo : ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment