Tuesday, March 11, 2014

KAMATI KUU CCM YARIDHIA RIDHIWANI KIKWETE KUGOMBEA CHALINZE

DODOMA,Tanzania
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Kada wa CCM, Ridhiwani Kikwete kuwa mgombea wake wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, marehemu Said Mwanamdogo.
Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya CCM kupitia Idara ya Itikadi na uenezi CCM, imesema wakati uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi huo utafanywa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kampeni za zitaongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa baada ya mchakamchaka mkali, kampeni za CCM zitafungwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Ifuatayo chini ni Taarifa Rasmi ya CCM
Imetayarishwa na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...