Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha alipokutana nao kutoa ufafanuzi kuhusiana na kutokuwepo kwa mpango wa kuikabidhi Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa wawekezaji kutoka Afrika Kusini kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila wiki nchini hivi karibuni.Picha kwa hisani ya TANAPA
----
Katika gazeti la Jamhuri Toleo Namba 129 Machi 25-31, 2014 kulikuwa na habari iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari “Nyalandu ‘auza’ Hifadhi” ambapo maelezo ya habari hiyo yaliitaja Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
No comments:
Post a Comment