Thursday, March 13, 2014

Samuel Sitta Ashinda Rasmi Nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Kwa Kupata Kura 487 dhidi ya Kura 69 za Hashim Rungwe ambapo Kura 7 Ziliharibika kati ya kura zote 563 zilizopigwa


  Wajumbe wakipiga kura  
  Aliekuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akishukuru kwa furaha muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi  wa nafasi hiyo kwa kura 469 dhidi ya mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita. Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu.Pia amempongeza mpinzani wake, Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo. 
 Picha Juu ni  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo
  Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo. Picha zote na Deusdedit Moshi, Dodoma.
Katibu wa Bunge Thomas Kashilila akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu kukamilika kwa uteuzi wa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa Bunge Maalum wa Katiba Ofisi Kwake Mjini Dodoma.Picha na Oweni-Bunge

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...