Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho
Mnadhimu Mkuu wa CCM kwenye Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin akizungumza jana mjini Dodoma kuhusu kutotambua maoni ya Baraza la Wawakilishi yaliyopelekwa na kwenyeTume ya Mabadiliko ya Katiba. Kushoto ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha. Picha na Emmanuel Herman
----
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho amekiri kuwasilisha waraka kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba na kupendekeza Zanzibar na Tanganyika kuwa na mamlaka huru, hatua ambayo imezua malalamiko miongoni mwa makada wa chama hicho ambao wamesema huo ni usaliti.
Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma, Kificho ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), alisema kimsingi waraka huo ulilenga kuipa nguvu Zanzibar kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano ili kujiimarisha kiuchumi.
Kauli ya Kificho inakuja wakati baadhi ya wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar wakiitisha mkutano na kutoa tamko la kumshutumu kwa kutoa mapendekezo hayo, wakisema ni kinyume na msimamo wa chama hicho.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.....
No comments:
Post a Comment