Matokeo Rasmi ya Kalenga:
Mgimwa Godfrey (CCM): 22,962 - 79.32%
Tendega Grace (CHADEMA): 5,853 - 20.22%
Minja Richard (CHAUSTA): 150 - 0.52%
Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juu na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo CCM imeshinda kwa mbali katika matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye jimbo la Kalenga mkoni Iringa, Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Godfrey Mgimwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ambapo CCM imeshinda kwa kura 22962 huku CHADEMA ikipata 5853 na chama cha CHAUSTA kura 150 Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kushinda katika kata zote kumi na tatu za jimbo hilo.
Watu wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura na hali ilikuwa ni ya utulivu kabisa na watu wengi waliopiga kura wameishukuru serikali na tume ya uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na kufanyika kwa uchaguzi wenye utulivu..(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAlENGA)Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akipiga picha na wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo wana CCM walifurika kushangilia ushindi huo mnono ambao CCM imeshinda kwa kishindo.
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
No comments:
Post a Comment