Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya juzi,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini, ambapo Wananchi hao walipiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo jana siku ya jumapili.
Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa, akiwa chini ya ulinzi wa baada ya kukamatwa kwa madai ya kukutwa akigawa rushwa kwa wapigakura juzi jioni katika Kijiji cha Kitawaya, Kata ya Luhota, wakati ikiwa ni siku ya mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga jana. Hadi tunakwenda mitamboni Rose alikuwa bado anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoa wa Iringa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya jana kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho, kwa taratibu nyingine za kisheria. Picha na Bashir Nkromo na Ahmed Michuzi
No comments:
Post a Comment