Thursday, March 13, 2014

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU VITAMBULISHO KWA WAANDISHI BUNGE MAALUM LA KATIBA

1 (6)Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na wabahabari (hawapo pichani) kuhusu utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa Habari kwenye shughuli za Bunge Maalum la Katiba.
2 (4)Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na wabahabari (hawapo pichani) kuhusu utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa Habari kwenye shughuli za Bunge Maalum la Katiba. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Vyombo vya Habari cha Idara hiyo, Vicent Tiganya.
Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO
………………………………………………………………………………..
Na Frank Mvungi-MAELEZO
SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari ( Press card) wakati wa Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo pekee kitakachowezesha  waandishi wa habari kutimiza majukumu yao vyema katika kipindi  chote cha bunge hilo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia  taarifa potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa  nchini.
Mwambene alibainisha kuwa  utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si  mgeni kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo.
Alisema vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari kutoka chuo kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na kanuani zilizowekwa.
Alisisitiza  kuwa utaratibu wa kutoa  vitambulisho kwa waandishi  habari upo  na ni wa kisheria  hivyo ni lazima ufuatwe.
Pia  alisema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata taratibu zote za kupata kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila kitambulisho hicho hataweza kufanya kazi  katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la katiba.
Alitoa wito kwa waandishi wa habari kujiendeleza katika taaluma ya uandishi wa habari kwa wale wasio na sifa za kupewa vitambulisho hivyo ili kuiniua Sekta ya Habari hapa nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...