KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI APOKEA MAGARI MAWILI KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA

DSC_0166Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya NIT.
DSC_0171Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
DSC_0173Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini Uingereza.
DSC_0183     Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya chuo hicho leo Asubuhi.
DSC_0185Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal liftkama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT), leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt.  Zakaria Mganilwa
DSC_0192Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Liftlililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Comments