Jana katika Mchezo wa soka wa kinyang'anyiro cha klabu bingwa Barani Afrika, uliozikutanisha timu za Yanga (Tanzania) na Al-Alhly (Misri) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (Tanzania), timu ya Yanga imepata ushindi wa goli moja.
Lakini cha kustajaabisha ni ripoti kuwa kabla hata ya kuanza kwa mtanange huo, baadhi ya mashabiki wa timu ya soka ya Simba ambayo ni wapinzani wa jadi wa Yanga, walianza kung'oa viti na kuvirusha upande walipokuwa wameketi washabiki wa Yanga.
Chokochoko hizo inaripotiwa kuwa zilitulia wakati mchezo ukiendelea, ila zikarejea tena mara baada ya Yanga kupata goli, saari hii ni mashabiki wa Simba tena waliovalia jezi za Simba walianza tena kung'oa viti na kuwarushia mashabiki wa timu ya Yanga waliokuwa wakishangilia. Tizama picha zaidi hapo chini.
No comments:
Post a Comment