Monday, March 10, 2014

GODFREY MGIMWA AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA MVUA KUBWA

2Mgombea  ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juu juu na wananchi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke Iringa vijijini huku kukiwa na mvua kubwa ambayo hata hivyo haikuzuia kuendelea kwa mkutano huo, wananchi wa kijiji hicho walionekana kuwa na hamu kubwa ya kumsikiliza mgombea huyo wa (CCM) walisikika wakisema “Nini mvua sisi tunataka sera tu, tunataka tusikilize maneno ya huyu mgombea wa (CCM)”3Mgombea  ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Wenda huku mvua kubwa ikinyesha kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu.4Mkutano ukiendelea huku wananchi wakimsikiliza wakiwa katika mvua kubwa5Wananchi hawa wakimsikiliza mgombea huyo wa CCM huku wakiwa wamejihifadhi katika moja ya mabanda ya biashara ndogondogo kijijini hapo.6Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu akimnadhi Bw. Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni kwenye kjiji cha Wenda kata ya Mseke.7Wananchi wakinyanyua mikono0 yao juu kuonyesha ishara ya kumkubali Bw. Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Saadani.9Msanii Dokii akiimba na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Tanangozi kata ya Mseke.10Wananchi wakiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni katika kijiji cha Tanangozi.11Mgombea  ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Saadani kata ya Mseke.12Umati uliohudhuria katika mkutano huo kijijini Saadani.13Umati uliohudhuria katika mkutano huo kijijini Saadani. PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...