KAMATI YA MAANDALIZI YA
MKUTANO WA DIASPORA NCHINI
UINGEREZA 2014
Kufuatia hatua ya Ubalozi
wa Tanzania nchini Uingereza kuunda kamati ya muda (Tanzania UK Diaspora Task
Force) itakayosimamia maandalizi ya Mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014,
tunapenda kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati hiyo kwa Watanzania waishio
Uingereza.
Kamati hiyo itakuwa chini
ya Uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga
akisaidiwa na Bw. Cleopa John katika
nafasi ya Katibu. Aidha Bi Maxine Brown
atashughulikia mawasiliano kati ya kamati na watanzania waishio nchini
Uingereza.
Wajumbe wengine wa Kamati
hiyo ni wafuatao:
Salim Amar: Makamu
Mwenyekiti
Mariam Mungula: Makamu
Katibu
Hassan Mussa: Mratibu wa
Wajumbe wa Kamati
Mchungaji Mathew Jutta: Mjumbe
Kassim Kalinga: Mjumbe
Amos Msanjila: Mjumbe
Allen Kuzilwa: Mjumbe
Sheikh Rashid Saleh: Mjumbe
Watanzania waishio
Uingereza mnaombwa kuunga mkono uongozi wa kamati hii katika kufanikisha mkutano wa Diaspora
mwaka huu 2014. Kwa kuanzia Watanzania mnaweza kutuma maoni kuhusu mnayotarajia
kuyaona kwenye Mkutano wa Diaspora mwaka
2014 kwa kujaza fomu ya utafiti iliyopo kwenye anuani ifuatayo : https://www.surveymonkey.com/s/5VVGK9Z
Aidha mawasiliano na Kamati
yanaweza kufanyika kupitia mitandao ya kijamii ifuatayo:
Facebook:
www.facebook.com/tanzaniauk
Twitter:
@tanzaniaukdiasp
Barua
Pepe: TanzaniaUKDiaspora@gmail.com
No comments:
Post a Comment