Pichani ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Deos Mndeme akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar mapema leo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Pichani Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara,Bwa.Fortunatus Kapinga akifafanua jambo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.Amesema kuwa Shirika la Posta limeanza utekelezaji mpango kabambe wa miaka kumi (2014-2023) ikiwa ni dira na mwelekeo wa kuliongoza shirika hilo liweze kujiendesha kibiashara,kubuni na kutoa huduma mbadala,kutumia teknolojia maridhawa na kukidhi mahitaji ya soko la huduma za mawasiliano jumuishi.Kushoto kwake ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania,Bwa.Deos Mndeme.
Tanzania,Bwa.Deos Mndeme.
Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Elias Madule akifuatilia mkutano huo akiwa sambamba na mdau mwingine wa shirika hilo la Posta.
Waandishi wa Habari wakisikiliza taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Viongozi wakuu wa Shirika hilo,katika mkutano uliofanyika mapema leo,ndani ya Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar.
No comments:
Post a Comment