Thursday, March 06, 2014

Askofu Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo asema msimamo wa Katoliki si Serikali tatu

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwaonesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, nakala ya gazeti la Mwanachi lililoandika habari kuhusu msimamo wa Kanisa juu ya suala la serikali tatu. Picha na Venance Nestory  
---
 Siku mbili baada ya Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoa waraka wa kulitaka Bunge Maalumu la Katiba kutopuuza mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, Askofu Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameibuka na kusema msimamo huo siyo wa Kanisa Katoliki nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kardinali Pengo pamoja na kukiri kuwa tume ilitoa maoni hayo, alikanusha kuwa taarifa zilizotolewa na moja ya magazeti kuwa msimamo wa Kanisa Katoliki ni serikali tatu.
“Maoni ya Tume hayawezi kuwa ni msimamo wa kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa misimamo yake na huwa inatolewa na Mwenyekiti wa TEC,” alisema.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea...

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...