Monday, January 14, 2013

YANGA YAWASILI DAR SALAMA, SASA NI SUMU ZA UTURUKI LIGI KUU



Wachezaji wa Young Africans wakishuka kwenye bus uwanja wa 
ndege wa Antalya tayari kwa kuanza safari ya kurudi Tanzania

Timu ya Young Africans Sports Club iliyokuwa imeweka kambi ya wiki mbili katika mji wa Antalay nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom na mashindano ya kimataifa tayari imeshatua nchini leo aflajiri.
Msafara wa watu 33 ukiwa na wachezaji 27 na viongozi 6 umewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa majira ya saa 10 kasoro alfajiri kwa shirika la ndege la Uturuki Turkish Air ambapo katika mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako aliongoza mapokezi hayo.
Young Africans iliweka kambi katika hoteli ya Fame Residence kwa kipindi chote cha mafunzo ambapo pia ilipata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu na timu kutoka barani ulaya katika nchi za Uholanzi, Uturuki na Ujerumani. 
Mara baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege bus la klabu liliwachukua wachezaji na viongozi tayari kwa kwenda kupumzika ambapo kocha mkuu Ernest Brandts ametoa mapumziko ya siku 2 kwa wachezaji kukaa na familia zao kabla ya kuanza mazoezi tena siku ya jumatano kujiandaa na ligi ku ya vodacom.

Mbuyu Twite, Didier Kavumbagu, Kabange Twite & Shadrack Nsajigwa
Ladislaus Mbogo, Jerson Tegete, David Luhende, Kelvin Yondani, Juma Abdul & Haruna Niyonzima

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...