Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi
akiwasili nchini usiku wa jana, kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi
alipokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa
tano unusu usiku.
Kesho
asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais
Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete
akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa
leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya
Kilimanjaro leo usiku(Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment