Na Shomari Binda
Musoma,
SHIRIKA la
Nyumba la Taifa (NHC) limetoa msaada wa ujenzi wa jengo la vyoo lenye matundu
14 katika Shule ya Msingi Mwisenge aliyosoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya Miaka 50 ya Shirika hilo.
Katika
hotuba yake ya uzinduzi wa Jengo hilo uliofanyika shuleni hapo,Meneja wa Huduma
kwa Jamii wa Shirika hilo Muungano Saguya alisema Shirika la nyumba la Taifa
kwa kutamba wajibu wake kwa Jamii linayo sera ya kusaidia Maendeleo ya Jamii
katika Nyanja mbalimbali.
Alisema
licha ya kuwepo changamoto mbalimbali katika Shule hiyo yenye historia kubwa
katika Taifa la Tanzania wamejaribu kupunguza changamoto hizo kwa kubolesha miundombinu
ya vyoo ambayo imeghalimu kiasi cha shilingi milioni 16 ili kuviweka katika
hali ya kuridhisha.
Saguya
alisema ili mtoto aweze kupenda shule pamoja na masomo ni wajibu kumuwekea
mazingira mazuri ambayo yatamfanya kila wakati atamani kwenda shuleni na
kujiepusha na utoro ambao unaweza kuzolotesha elimu.
“Kila mmoja
wetu anafahamu kuwa ili Nchi yoyote iendelee inahitaji elimu kwa watu
wake,Taifa letu halikadharika limekuwa likijitahidi kuwekeza katika elimu ili kuweza
kwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya uchumi na teknolojia ya Dunia.
“Hivi sasa
katika ukanda wa Afrika Mashariki tumeungana na Nchi jirani katika Nyanja za
kiuchumi,hivyo itoshe kusema hatuwezi kushindana na Nchi hizi jirani kama
tutapuuzia kuweka mkazo katika kuwekeza zaidi katika Elimu,”alisema Saguya.
Alisema NHC
ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mahala pazuri pa kujistiri imeona itengeneze
vyoo vya kisasa katika shule hiyo kwa kuwa shule isipokuwa na vyoo imara
huwafadhaisha na kuwadhalilisha wanafunzi wengi.
“Shirika
lina kila sababu ya kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere kama mnakumbuka NHC
lilikuwa Shirika la kwanza kuanzishwa na Mwalimu Mwaka 1962 ikiwa ni Mwaka
mmoja baada ya Uhuru.
“Mwalimu
Nyerere alithamini sana vitu vitatu katika kuleta utu wa Mwanadamu vitu ambavyo
ni pamoja na nyumba,mavazi na malazi hivyo tunatoa mchango huu kama shemu ya
kuadhimisha miaka 50 na kuenzi jitihada za Mwalimu Nyerere la kulianzisha
Shirika hili,”aliongeza.
Katika
taarifa iliyotolewa na Meneja NHC Mkoa wa Mara Jocton Matogo juu ya ujenzi huo
alisema ujenzi ulianza julai 2012 na kukamilika oktoba 2012 ikiwa na matundu
saba kwa Wasichana na matundu saba kwa wavulana.
Alisema mradi wa choo cha wanafunzi katika shule hiyo
uliibuliwa na uongozi wa Shirika Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na uongozi wa
shule baada ya kutathimini mahitaji ya haraka na kutimiza sehemu ya miradi ya
huduma ka Jamii inayotolewa na Shirika hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Shule
hiyo Mathias Buguti amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa msaada waliotoa
katika shule hiyo kwa kuwa ilikuwa ni hitaji lao kubwa kwa sasa kwa kuzingatia
wingi wa wanafunzi katika shule hiyo. SOURCE: AUGUSTINE MGENDI KATIKA BLOGU YAKE YA http://mwanawaafrika.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment