Friday, January 11, 2013

70 waibuka washindi Vodacom

003.NOKIA da1bc

Taarifa kwa vyombo vya habari
Wateja 70 waibuka washindi kwenye droo kubwa ya Promosheni ya Patapata na Nokia Ushinde'
Dar es Salaam, Januari 11, 2013 ... Washindi takribani 70 wamepatikana kupitia droo kubwa ya Patapata na Nokia Ushinde' ambayo imechezeshwa ikishirikisha wateja wote walionunua bidhaa hizo tangu kuanza kwa promosheni hiyo mnamo mapema mwezi Desemba mwaka 2012.

Katika Droo hiyo iliyoendeshwa na Nokia kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, wateja 20 wameibuka washindi na kujinyakulia zawadi za simu aina ya Nokia Lumia 900, wengine 20 wamezawadiwa Nokia Lumia 800 huku wengine 30 wakiibuka na Nokia 808.
Miongoni mwa wateja waliopatikana katika droo hiyo ya moja kwa moja ni pamoja na Farhia Hassan mkazi wa Dar es Salaam akiyejinyakulia Nokia Lumia 900, mwingine ni Dennis Katunzi kutoka Mwanza aliyezawadiwa Nokia Lumia 800 huku Fidel Ngowi kutoka Dar es Salaam akipata Nokia 808.
Droo hiyo kuu ya kuhitimisha promoshni hiyo tangu Vodacom na Nokia walipoizindua , imechezeshwa moja kwa moja kwenye Makao Makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam, na kusimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (Tanzania Gaming Board).
Akizungumza wakati wa promosheni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Kelvin Twissa, amewataka washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali na kujulishwa kupitia simu zao za mikononi wafike kuchukua zawadi zao kati ya Januari 11 na 14 katika maduka ya vodacom nchi nzima.
Twissa amefafanua kuwa droo hiyo ambayo imemalizika, imewezesha mteja mmoja mmoja kujipatia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 1000 tangu ilipoanza mwezi mmoja uliopita.
Naye Meneja wa Biashara wa Nokia, Ellen Lupilli, amewataka washindi waliopatikana kuwa mabalozi na mashuhuda kwa wengine ambao bado wanamtazamo hasi dhidi ya promosheni kama hizo.
Aidha, amewashukuru watanzania waliojitokeza kwenye promosheni hiyo, ambapo kwa niaba ya Nokia ameahidi kuzidi kuboresha huduma kwa maslahi ya wateja wake.
"Nawasihi wateja wa bidhaa za Nokia kuendelea kuzipenda bidhaa zetu, na zaidi jitokezeni kwa wingi wakati mwingine tunapoandaa promosheni kama hizi, inaweza kuwa bahati yako," amesema Lupilli.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...