Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bw. Kelvin Twissa, akionesha moja ya simu aina ya Nokia ambazo zinashindaniwa katika shindano la PATAPATA na Vodacom na Nokia linaloisha leo hii, katikati ni Meneja Masoko wa Nokia, Ellen Lupilli na Mkuu wa kitengo cha vifaa vya mawasiliano na wateja wa Vodacom, Mgopelinyi Kiwanga.
---
Ile promosheni ya PATAPATA ya Vodacom na Nokia iliyozinduliwa mapema
mwezi Disemba mwaka jana 2012 leo hii Alhamisi tarehe 10 Januari 2013
inafikia mwisho wake ambapo kila mteja atakayenunua simu za Nokia leo na
kisha kutuma SMS yenye maneno NOKIA ikifuatiwa na namba ya kuponi
kwenda 15544 atajishindia simu ya Nokia.Promosheni hii ya kipekee na ya aina yake ilizinduliwa mahususi kuwawezesha wananchi siyo tu kujipatia simu za kisasa za Nokia kwa bei nafuu bali pia kuwanufaisha na ofa ya BURE kutoka Vodacom ya dakika za maongezi, SMS na vifurushi vya intaneti. Pia kila mteja aliyenunua simu za Nokia kwenye kipindi cha promosheni alikuwa anabahatika kujishindia mojawapo ya zawadi mbalimbali za papo hapo kutoka Nokia. Zawadi hizi za papo hapo ni pamoja na t-shirts, Monsters headphones, Bluetooth BH 111, Bluetooth BH 112, Portable chargers, Nokia Asha 202, Nokia Asha 302, Nokia Asha 306, Nokia Asha 308 na Nokia Lumia 610.
Hadi hivi leo, zaidi wa wateja 300 wameshajishindia zawadi mbalimbali za papohapo na namba zao za simu kuingizwa kwenye droo kubwa.
Kesho Ijumaa Januari 11, 2013, itachezeshwa droo kubwa ya kuwapata washindi 70 watakaojishindia zawadi za simu za kisasa za Nokia 808 pure view, Nokia Lumia 800 na Nokia Lumia 900. Kwa hiyo tunapenda kuwasihi wateja wetu walioshiriki kwenye promosheni hii kuhakikisha namba zao za simu zinakuwa wazi ili iawapo watabahatika kushinda basi wasiweze kukosa zawadi zao hizi.
No comments:
Post a Comment