Monday, January 07, 2013

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa  akisoma ripoti ya mkoa wa Tabora kwa Rais Jakaya Kikwete mara baada ya Rais Jakaya Kikwete  kuwasili Mkoani Tabora Kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.Picha na IKULU

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...