Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Sajuki kama ambavyo anajulikana na wengi kwa sinema zake za kashkash alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu mpaka kufikia hatua ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi (Ref: Jamani inasikitisha hali ya afya ya Sajuki mme wake Wastara )
Sajuki ambaye ameacha mjane ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mnamo mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa. Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa kina Wastara.
Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto
Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichopelekea wasanii wenzake na watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia Sajuki (Ref: Jamani tumsaidie msanii SAJUKI ).
Waasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumfanya aweze kwenda India kwa matibabu zaidi.
Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta nyuso za furaha na amani miongoni mwa watanzania (Ref: PICHA: Sajuki shavu dodo, sasa Mungu mkubwa ).
Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi.. na hii alikiri kwenye kipindi cha 'Mkasi' kinachoendeshwa na kituo cha televisheni cha EATV.
Sajuki ambaye ni mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa Tanzania.
Sajuki kwa kusaidiana na mkewe walifungua kampuni ya productions kwa ajili ya filamu (movies) za hapa hapa nchini.
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Wednesday, January 02, 2013
TANZIA: Msanii Sajuki afariki dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment