Katibu Mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana akihutubia ngaruka
Dk Asha-Rose akihutubia Nguruka
Nape Nnauye akihutubia Ngaruka
Kinamama katika mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza mkoani
Kigoma, wakipokea kwa shangwe msafara wa Kinana na ujumbe wake
ulipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Juma Kilabuka na Hasani Kankwi wa mjini mdogo wa Nguruka wakifurahia msafara wa Kinana ulipofika katika mji huo
Kinana
akisalimia wananchi katika mji mdogo wa Nguruka , Uvinza mkoani Kigoma
baada ya msafara wake kuwasili katika mji huo kwa ajili ya mkutano wa
hadhara.
Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka, Asha
Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake
ulipowasili Nguruka mkoani Kigoma, Januari 28, 2013.
Kinana akiaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara
katika mji mdogo wa Nguruka, wilayni Uvinza mkoani Kigoma. Kushoto kwake
ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
Dk.
Asha Migiro akiwa katika matembezi kuingia mjini mdogo wa Nguruka
wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM.
Kushoto ni Asha Baraka.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji
mdogo wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kwenda kwenye mkuytano
wa hadhara wa CCM, Nguruka, Januari 28, 2013. Pembeni yake ni Asha
Baraka
Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea
ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akimtembeza Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na ujumbe wake kushuhudia hali ya
ujenzi wa daraja hilo ilivyo, Januari 28, 2013, wilayani Uvinza mkoani
Kigoma. Kwa mujibu wa You mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na
unatarajiwa kukamilika Aprili mwaka huu. Wengine ni Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa wa Umoja wa
Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne) na Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye (wapili kushoto) . Kinana na ujumbe wake wapo mkoani
Kigoma kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha sherehe za miaka 36 ya
CCM zitakazofanyika Januari 3, 2013.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Khalidi wakati
akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kushoto ni Meneja mradi wa
ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Yong.Picha Zote na Bashir Nkromo-Idara ya itikadi na Uenezi-CCM
----
CHAMA Cha
Mapinduzi(CCM), kimesema kuwa wananchi wa Mtwara wanayo hoja hivyo Serikali inatakiwa
kuwasikiliza na kutoa majibu sahihi.
Pamoja na
hayo chama hicho kimesema kuwa kinachoonekana hivi sasa nyuma ya sakata hilo
kuna watu wanafanya uhaini, uhalifu na kila aina ya hujumu jambo ambalo
wanaitaka Serikali kuchukua hatua kali za kuhakikisha wote wanojihusisha na
uhalifu huo wanachukuliwa hatua.
Kauli hiyo
ilitolewa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ikiwa ni
msimamo wa chama chao katika sakata hilo.
Mjadala wa
gesi ya Mtwara kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam umekuwa gumzo kubwa huku
wananchi wakiitaka Serikali kuwaeleza watanufaika vipi na gesi hiyo kabla ya
kunufaisha maeneo mengine.
Kinana
alisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuhakikisha inatumia nafasi yake kuzungumza
na wananchi wa Mtwara katika kupata suluhu ya suala hilo kwani wana hoja za
msingi ambazo zinataka majibu.
“Msimamo
wetu kama chama, tunataka Serikali kukaa na wananchi hao na
kuwasikiliza.Tunahitaji kuona Serikali inatoa majibu ambayo yatakuwa sahihi na
kumaliza tofauti iliyopo sasa,”alisema Kinana.
Pamoja na
hayo alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona hali ya uvunjifu wa amani
inayofanywa na baadhi ya watu ambao wameamua kuingia mtaani na kuiba, kupora
mali na kuharibu nyumba za watu kwa kuzichoma moto.
Alisema
kuwa CCM inaona ni wakati mzuri kwa Serikali kuwadhibiti wote ambao wanatumia
mwanya huo kufanya uhalifu huo ambao haukubaliki huku akisisitiza umuhimu wa
wananchi kusikilizwa.
Alisema
mtazamo wa chama chao ni kwamba kuna jambo ndani ya suala hilo maana gesi
inatakiwa kujadiliwa kwa njia ya amani kupata suluhu kuliko mali za watu
kuharibiwa na kufanywa kwa uhalifu ambao hauvumiliki.
No comments:
Post a Comment