Friday, January 11, 2013

Wanamuziki wa Injili Bwana na Bibi Mbasha watua London, Uingereza na kutembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Uingereza


Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwa Wanainjili hao Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha. Wanainjili hao wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading na wanatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Ijumaa 11/01/2013
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Bishop Irungu) na Bibi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi jana. Bwana na Bibi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili. Source: Hakingowi.blogspot.com

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...