Wednesday, January 16, 2013

Wazee waasisi wa CCM kutoka mkoani Singida Wamtembelea Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula


Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula (kushoto) akiwasikiliza Wazee waasisi wa CCM kutoka mkoani Singida, Kutoka kushoto, Sumbu Galawa, Alhaji Mahami Rajabu Kundya na  Mujengi Gwao Makamu, walipomfikishia ujumbe wao maalum, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
 Mzee Sumbu Galawa akimkabidhi ujumbe maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pilip Mangula, wakati yeye Wazee wenzake wa CCM kutoka mkoani Singida, Alhaji Rajabu Kundya (wapili kulia) na Mujengi Gwao (watatu kulia) walipofika Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, kuwasilisha ujumbe huo.
.Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phili Mangula akimshukuru Mzee Sumbu Galawa, baada ya kupokea ujumbe uliowasilishwa kwake na Wazee wa CCM kutoka mkoani Singida, Ofisi jana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
Mangula akizungumza na Wazee wa CCM kutoka mkoa wa Singida, waliofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba Dar es Salaam, kumpa ujumbe maalum wa kuimarisha chama. Kushoto ni Mzee Sumbu Galawa na kulia ni  Alhaj Mahami Rajabu Kundya na  Mujengi Gwao.Picha zote na Bashir Nkoromo, Uenezi-CCM

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...