Sunday, January 27, 2013

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Anusurika Kwenye Ajali Mkoani Morogoro

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa
Gari la  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali iliyotokea leo asubuhi.
-- 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa Mh. Edward Lowassa amenusurika kifo,baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.

Gari hilo la Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa liligongwa na basi la Morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari lakini dereva wa  Mh. Lowasa kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa  mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva na hakuna aliyejeruhiwa.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa na msafara wake aliendelea na safari hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala ambapo yeye na Marafiki Zake Wamechangia Shilingi Milioni 18

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...