Wednesday, January 16, 2013

MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU NA WAKUU WA MIKOA WATOA MAONI YAO JUU YA KATIBA MPYA

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yaokuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Nyamrunda akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiongea katika mkutano kati ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.
  Mawaziri Steven Wassira, Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika na Prof. Sospeter Muhongo wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia akiongea katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abass Kandoro, Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma) na Bi. Chiku Galawa (Tanga).
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Al-Shymaa Kway-Geer, Bw. Humphrey Polepole na Bi. Riziki Mngwali wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Mawaziri uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa nchini wakipata maelezo kuhusu mfumo wa uhifadhi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya yanayowasilshwa katika Tume kwa maandishi kutoka kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bi. Flora Mkonya  katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia(Mtwara), Bw. Abass Kandoro (Mbeya), Bi. Chiku Galawa (Tanga).na Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma).Wakuu hao wa mikoa pia waliwaslisha maoni ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Katiba Mpya.Picha na Tuma ya Mabadiliko ya Katiba

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...