Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa
moja ya barabara zilizojengwa na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo
kuhakikisha kama barabara hiyo imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa
kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo
kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema fedha za Serikali
katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha zilizotumika,
alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali katika
mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani
Rukwa.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo
chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi
karibuni. Katika ukaguzi huo alibaini mapungufu mbalimbali katika ujenzi
huo na kuagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha mapungufu hayo
yanaondolewa. Aliitaka pia halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi za
Serikali kuepusha minong’ono inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji
mbovu wa baadhi ya watendaji Serikalini.
Mhe. Agrey
Mwanri akiweka jiwe la msingi kiwanda cha unga cha Malangali
kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani mapema hivi leo. Kwa sasa Mkoa wa
Rukwa una viwanda vitatu vya unga vinavyomiliwa na wawekezaji wa ndani.
Naibu wa
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Agrey Mwanri akikagua kiwanda cha unga cha Malangali
Mjini Sumbawanga leo alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuweka
jiwe la msingi.
Mhe.
Mwanri akizungumza na wakazi wa Mji wa Sumbawanga katika Stendi kuu ya
mabasi ya Mjini hapo ambapo alipokea kero mbalimbali ikiwepo ubovu wa
miundombinu ya umeme na barabara katika stendi hiyo. Aliuagiza uongozi
wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi hao
kuskiliza kero zao zote pamoja na kuzitaftia ufumbuzi na kumpelekea
taarifa ya utekelezaji.
Katika
hali isiyotegemewa msafara wa Mhe. Mwanri ulipowasili katika kijiji cha
Mlanda katika Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya Mkutano wa hadhara
ulikuta msiba ambapo walishiriki na kutoa ubani ambapo Mhe. Mwanri
alitoa laki moja na alfu mbili na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini
CCM ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa ya CCM (NEC) kupitia
Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal alikabidhi shilingi alfu hamsini.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment