Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
AZAM FC imeingia
Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu, baada ya kuifunga Simba SC kwa penalti
5-4, kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 120 usiku huu kwenye
Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Hadi mapumziko, Azam FC
walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Mkenya, Humphrey Mieno
dakika ya 10, akiunganisha kwa kichwa kona maridadi iliyochongwa na kiungo
mzalendo, Ibrahim Mwaipopo.
Azam ilishambulia zaidi
baada ya bao hilo, kabla ya Simba kuzinduka dakika tatu baadaye na kuanza
kushambulia pia.
Mchezo huo ulisimama
kwa dakika tano kuanzia ya 14 hadi 19 kutokana na umeme kukatika uwanjani hapo,
hali iliyolazimisha kuwashwa kwa Jenereta.
Kipindi cha pili Simba
walibadilika mno kiuchezaji na kuanza kutawala mchezo jambo ambalo liliwasaidia
kupata bao la kusawazisha dakika ya 78, ambalo lilifungwa na Rashid Ismail. PICHA NA HABARI KUTOKA kwa http://bongostaz.blogspot.com/2013/01/simba-na-azam-katika-picha-usiku-huu.html
No comments:
Post a Comment