Sunday, January 27, 2013

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Sarakikya, ChengeWatoa Maoni Yao Juu ya Katiba Mpya

Jumapili, Januari 27, 2013: Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Mrisho Sarakikya akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Wajumbe waTumeya Mabadiliko ya Katiba walioongozwa na Mwenyekitiwa Tume hiyo Jaji, Joseph Warioba (kulia). Wajumbe wa Tume walikuta na Rais huyo mstaafu (kulia)jana (jumamosijanuari 26, 2013) ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akibadilisha mawazo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kulia Dkt. Salim Ahmed (kulia) Salim na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (katikati). Wajumbe wa Tume walikuta na Rais huyo mstaafu (kulia)jana(jumamosijanuari 26, 2013) ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Mhe. Andrew Chenge akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika jana jumamosi januari 26, 2013) katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu AugustinoRamadhani.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...