Wednesday, October 15, 2014

AIRTEL YAKARABATI DUKA JINGINE KISIWANI ZANZIBAR

1aMkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi akizungumza  jambo
wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel kisiwani
Zanzibar .Akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel
Tanzania, Adriana Lyamba na Maneja wa Kanda ya Zanzibar Mariam Yussuf.
2aMkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(kushoto) akimwelekeza jambo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mjini
Magharibi , Abdallah Mwinyi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa duka
la huduma kwa Wateja kisiwani Zanzibar ,wakishuhudiwa na wageni
wengine waalikwa.
3aMkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(kushoto) akimwelekeza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mjini
Magharibi, Abdallah Mwinyi jinsi huduma ya Airtel money ilivyoboreshwa
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja
kisiwani Zanzibar  .
4aMkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi akikata utepe kuashiria

uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja la Airtel kisiwani
Zanzibar(Kushoto) Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania,
Adriana Lyamba (kulia) Maneja wa Kanda ya Zanzibar Mariam Yussuf.
…………………………………………………………
• Wateja kufurahia ubora wa juu wa huduma kutoka Airtel kisiwani Zanzibar.
Airtel Tanzania  imefungua duka lake la kisasa  kisiwani Zanzibar
lililopo mtaa wa Mlandege lenye uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 100
kwa siku.
Ni duka la kisasa ambalo lipo karibu na  wateja lenye kurahisisha
maisha ya wateja wote wa Airtel kisiwani Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo Mkurugenzi kwa huduma kwa
wateja , Bi Adriana Lyamba alisema, “kwamba kupanua  kwetu kwa huduma
za mtandao kwa wateja wetu ni ishara  tosha ya kuonyesha ni jinsi gani
Airtel inajali wateja wake na kuwapatia wateja wetu huduma bora na za
kibunifu.
“Ni juhudi zetu  na  mafanikio yetu ya kuwa na wateja zaidi ya milioni
9 tulionao ndio yanayotufanya tuweze kuwashukuru wateja wetu kwa
kuwapatia huduma nzuri zenye Kiwango cha juu. Kwa huduma tunazozitoa
kupitia maduka yetu yaliyoenea hapa nchini maduka haya yanauwezo wa
kutoa huduma zenye kiwango cha juu  yanayotoa huduma kwa masaa mengi
na kutoa huduma nzuri kwa wateja. Uzinduzi wa maduka yetu ni mafanikio
makubwa kwetu na hii ni shukurani yetu kwao kwa kuwaonyesha ni jinsi
gani tunawajali wateja wetu.
Hafla hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa  Mjini Magharibi Abdallah
Mwinyi, ambaye aliipongeza Airtel kwa ajili ya kuleta huduma zake
karibu na watu wa Zanzibar.
“Mbali na kutatua matatizo ya wateja, mtazamo huu mpya wa duka hili ni
maendeleo tosha kwa wakazi wa Zanzibar kwani huduma zinazotolewa hapa
ni za kiwango kizuri na uwezo mkubwa ambapo wateja wa Airtel wamekuwa
wakihitaji hapa kisiwani Zanzibar. alisema.
Mwinyi alisema kuwa, huduma mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na
Airtel kuanzia , ujumbe, Inteneti , usajili, huduma za Airtel Money
ambazo zinarahisisha maisha ya wananchi katika jamii. “Huduma hizi
zinaleta matokeo mazuri katika namna ya kufanya biashara na kuboresha
maisha ya maelfu ya wakazi wa Zanzibar na mamilioni ya Watanzania kwa
ujumla,” aliongeza Mwinyi.
Kama sehemu ya huduma nzuri , Airtel tayari imekarabati maduka mengine
katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Bukoba, Mbeya, Mtwara, Dodoma,
Mwanza, Tabora na leo hapa Zanzibar.
Maduka ya Airtel  yataendelea kutoa huduma mbali mbali zenye kiwango
cha juu na upatikanaji wa bidhaa zake kama vile modems, simu, malipo
ya bili,huduma za Airtel money na huduma nyingine nyingi
Tumewekeza kwa kiwango kikubwa  katika mtandao wetu ili kuhakikisha
wateja wetu wanapata huduma sahihi na ya kiwango cha juu.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...