TAARIFA RASMI
Katika gazeti la Jamhuri la Jumanne Agosti 19 – 25, 2014 ISSN No. 1821-8156 Toleo No. 150, zilichapishwa taarifa potofu zenye kichwa cha habari;
KASHFA IKULU;
· Nyalandu atumia Leseni ya Rais kuua wanyamapori 704 bure,
· Watakaouawa wamo pia tembo 8, chui 8, Simba 8, ndege,
· Wauaji ni Wamarekani marafiki wa Waziri wa Maliasili.
I.
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwafahamisha Umma kuwa, tuhuma hizi si za kweli. Tuhuma hizi zimetolewa na watu wenye nia ovu na zimelenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu, kumshushia Heshima, kumdhalilisha kwa umma ili kumpunguzia dhamira, malengo na kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kwamba Familia ya Freidkin ilipewa Leseni Maalum/Leseni ya Rais (Special License/President’s License) ya kuwinda kwa mujibu wa Kifungu cha 58 (1) cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 ikisomwa kwa pamoja na Tangazo la Serikali Na. 273 la mwaka 1974 ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori baada kupata ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya Wanyamapori kutoa kibali maalum kwa malipo au bure. Aidha, kibali hicho hutolewa baada ya Waziri kuridhika kwamba kibali hicho kina maslahi kwa taifa na hakikinzani na sheria na mikataba ya kimataifa kama CITES.
Kufuatana na Kifungu hicho cha 58 (1) Leseni Maalum hutolewa kwa mtu yeyote kwa masilahi ya kitaifa ikiwemo:-
1. Utafiti wa kisayansi
2. Makumbusho
3. Elimu
4. Utamaduni na
5. Chakula wakati wa dharura
1. Utafiti wa kisayansi
2. Makumbusho
3. Elimu
4. Utamaduni na
5. Chakula wakati wa dharura
Maslahi ya taifa ni pamoja na leseni kutolewa kwa watu mashuhuri kama vile Wakuu wa nchi, Wafalme, Malkia, Wakuu wa dini pamoja na watu ambao katika utendaji wao wametoa michango yenye manufaa maalum kitaifa au michango mikubwa katika shughuli za uhifadhi wa wanyamapori.
Katika utaratibu huu, kwa mwaka 2013 hadi sasa, Leseni ya Rais zimetolwa kwa watu wafuatao:-
Na. Jina Kibali Na. Kampuni iliyowindisha Bure/Malipo
1 H.H. Sheikh Abdullah Mohamed Buli Al Hamed 000000657 cha 22/8-6/09/2013 Kilombero North Safaris/Green Mile Safaris Bure
2 H. H Sheikh Mohamed Rashid Al Maktoum 0000676 cha 16/01 – 26/01/2014 Ortello Business Corporation (OBC) Bure
3 Familia ya Freidkin ya Watu wanane 00006678-85 za 1-21/08/2014 Tanzania Game Trackers Safaris Ltd Kwa malipo
4 Kiongozi wa Bohora Duniani Bure

Familia ya Freidkin imekuwa na sifa ya kupewa Leseni ya Rais kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa katika shughuli za uhifadhi wa Wanyamapori kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini iliyopita bila kukoma.
Familia ya Freidkin imekuwa ikitoa mchango huo kupitia Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii iitwayo Tanzania Game Trackers Safaris Ltd. Pamoja na Asasi yake iitwayo Freidkin Conservation Fund (FCF tangu miaka ya 1990).
FCF imekuwa ikitoa michango mikubwa hususan ya kukabiliana na ujangili.
Bw. Freidkin kwa kupitia Taasisi hii amekuwa akichangia na hata kushiriki katika shughuli za kuzuia ujangili na shughuli za kijamii kwa kufanya yafuatayo:-
Bw. Freidkin kwa kupitia Taasisi hii amekuwa akichangia na hata kushiriki katika shughuli za kuzuia ujangili na shughuli za kijamii kwa kufanya yafuatayo:-
No comments:
Post a Comment