Wahitimu wa elimu ya sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakiwa wakimptia maua Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake wa kusaidia watoto wa kike wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Msanii Vicky Kamata akiimba wimbo wa kumpongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa juhudi za kumkomboa mtoto wa kike kielimu wakati mahafali ya pili Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani yaliyofanyika juzi.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migoro(kulia) akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani Ulizeni Ngonyani katika mahafali ya pili yaliyofanyika jana
.Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakifurahia na jambo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika juzi.
Picha namba 8892 ni Baadhi ya wake za viongozi waliohudhuria sherehe hiyo.
.Picha na Magreth Kinabo, Maelezo
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro (katikati ) akizindua zahanati kwa ajili ya matibabu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati mahafali ya pili yaliyofanyika juzi.
Wahitimu wa elimu ya sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wakiimba wimbo wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
No comments:
Post a Comment