Wednesday, October 15, 2014

RAIS KIKWETE AWAPA URAIA WAKIMBIZI WA BURUNDI 162,156 MJINI TABORA

1aRais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora leo. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
2aMwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
4aMsoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
5aSehemu ya wakimbizi wa Burundi 162,156 ambao sasa ni raia wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwapa uraia katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo. Rais Kikwete amewataka raia hao wapya wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
6aRais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...