Thursday, October 30, 2014

TAARIFA YA KIFO CHA MEJA JENERALI AI MFUSE

unnamed
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa akipata matibabu.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo. 
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...