Thursday, October 16, 2014

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘WELCOME PACK’ MKOANI IRINGA

1aMkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Dkt. Christine Ishengoma akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Tigo kanda ya kusini Bw. Jackson Kiswaga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kifurushi kipya cha tigo cha welcome pack mkoani Iringa, kifurushi hicho kitamwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakiak 20, mb175,sms bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.2a   Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dkt. Christine Ishengoma akipata maelezo toka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Tigo juu ya huduma zitolewazo ndani ya basi la kidijitali la Tigo kwenye uzinduzi wa kifurushi kipya cha Tigo welcome pack mkoani Iringa. Kifurushi inatoa muda wa maongezi wa dakika 20, mb175, sms bila kikomo na shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.4a  Msanii Lucas Mhavile maarufu Joti akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.5a  Msanii Lucas Mhavile maarufu Joti akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.6qMkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dkt. Christine Ishengoma akipata maelezo toka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Tigo juu ya huduma zitolewazo ndani ya basi la kidijitali la Tigo kwenye uzinduzi wa kifurushi kipya cha Tigo welcome pack mkoani Iringa. Kifurushi inatoa muda wa maongezi wa dakika 20, mb175, sms bila kikomo na shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.DSC_0014Msanii Slivery Mujuni maarufu Mpoki akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa waliofurika kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.DSC_0016Msanii Joseph Haule maarufu Professor J akiwapa burudani wakazi wa mkoa wa Iringa waliofurika kwenye uwanja wa samora hii ni sehemu ya burudani zitolewazo kwenye kampeni ya kifurushi kipya cha Tigo cha welcome pack.
………………………………………………….
Tigo Tanzania leo imezindua kifurushi kipya cha ‘Welcome Pack’ ambayo itawezesha wateja wake kupata huduma ya intanet, SMS, na kupiga simu kwa bei nafuu. Uzinduzi wa kifurushi hichi pia inaenda sambamba na kampeni maalum yenye nia ya kuwaelimisha watu na kuwapa fursa ya kushuhudia bidhaa na huduma mbali mbali itakayofanyika katika mikoa 10 nchini. 
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hii iliyofanyika katika Uwanja wa Sokoine mkoani Iringa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dk. Christtine Ishengoma aliipongeza sana mchango wa Tigo katika kuleta maendeleo kwa watu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kwa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano ambayo imekuwa kama kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu hususan wa mikoani. 
“Suala la kwamba kifurushi cha Welcome Pack itawapatia wananchi fursa ya kupata dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za kuperuzi katika intanet, SMS zisizo na kikomo na Tsh 500 katika akaunti yake mpya ya Tigo Pesa, yote hayo kwa Tsh 1000 kama gharama ya kununulia laini ya simu itawapatia wateja nafasi nzuri ya kuwasiliana zaidi na kwa gharama nafuu,” alisema Dk. Ishengoma. 
“Napenda kuchukua nafasi hii kutoa rai kwa wananchi wote wa Iringa kuchangamkia kifurushi hiki maalum kutoka Tigo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii hapa mkoani nap engine. Tumieni muda wa maongezi, intanet, SMS za bure kuwezesha miamala ya kibiashara na kupata elimu ya kibiashara mtandaoni, vitu ambavyo mwisho wa siku vitawasaidia kuongeza uzalishaji na kupata masoko ya kibiashara,” alisema Mkuu huyo wa mkoa. 
Dk. Ishengoma pia alisifia kampuni ya Tigo kwa hatua yao yakuanzisha Basi la Kidijitali la Tigo lenye uwezo wa kuwapatia Watanzania elimu kuhusu bidhaa na huduma mbali mbali zitolewazo na kampuni hiyo kama Tigo Kilimo, Tigo Bima, Tigo Pesa, Application ya Hesabati kwa wanfunzi wa sekondari, na Facebook ya Bure kwa Kiswahili. 
“Ni dhahiri kwamba kuja na wazo hili la kibunifu litasaidia kuongeza elimu ya kidijitali kwa Watanzania hasa hasa wale wa vijijini, ambayo moja kwa moja inachangia katika ufanikishwaji wa dira ya kampuni yenu ya kuwezesha maisha ya kidijitali nchini,” alisema Dk. Ishengoma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda za Juu Kusini, Joseph Kiswaga alisema kwamba kampuni ya Tigo inayofuraha kutangaza uzinduzi rasmi wa kampeni ya Welcome Pack ambayo itawazawadia wateja wa Tigo watakaojiunga na mtandao huo kwa mara ya kwanza kwa kununua laini za Tigo. 
Alisema, “Kampeni ya Welcome Pack itakuwepo kwa muda wa miezi mitatu, ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la Tigo la Kidijitali litatembelea miji 70 na vijiji Zaidi ya 100 ndani ya mikoa 10 tofauti ikiwemo Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Mtwara.”
“Misafara hii yataambatana na tamasha la muziki katika kila siku ya mwisho wa msafara utakaofanyika kila Jumapili. Wasanii wa Bongo Fleva watakaotoa burudani ni pamoja na Profesa J, Joh Makini, Shah, Mheshimiwa Temba na Chege, Madee na Izzo Business. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni nyote,” alimalizia kwa kusema Kiswaga.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...