Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..
Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .
No comments:
Post a Comment